BAGHDAD:Moto wazuka kwenye kituo cha jeshi la Marekani nchini Irak
11 Oktoba 2006Matangazo
Moto uliozuka kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani mjini Baghdad ulisababisha miripuko kadhaa mikubwa.
Habari zinasema moto huo ulitokea kwenye bohari ya silaha, lakini hadi sasa hakuna habari iwapo umesababisha madhara yoyote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Marekani,miripuko hiyo ilisababishwa na joto kali.