BAGHDAD:Hali nchini Iraq
30 Agosti 2007Matangazo
Kiongozi wa kidini wa madhehebu ya washia Muqtada al-Sadr ametangaza kusimamisha shughuli zote za wanamgambo wake wa jeshi la Mahdi kwa muda wa miezi sita.
Sadri alitoa amri hiyo hapo jana baada ya siku mbili za mapambano kwenye mji mtakatifu wa Karbala kati ya vikosi vya usalama na jeshi hilo la Mahdi.
Zaidi ya watu 50 waliuwawa na maelfu ya waumini wengine kukimbia sherehe hizo za kidini zilizokuwa zinafanyika kwenye mji huo.Kufuatia ghasia hizo waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki alilazimika kutangaza amri ya kutotoka nje katika mji huo pamoja na kutuma wanajeshi wa kuweka amani.Katika tukio jingine watu sita waliuwawa kwenye mapigano kati ya makundi hasimu ya washia mjini Hilla.