1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Watuhumiwa wa Al Qaeda mbaroni

12 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDMD

Waasi wa Iraq wamewauwa raia wanane na kapteni mmoja wa polisi katika mashambulizi nchini kote leo hii wakati operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya ulinzi ya Iraq na Marekani ikiwatia mbaroni madarzeni ya watuhumiwa wa kundi la Al Qaeda.

Jeshi la Marekani limetangaza kukamatwa kwa watuhumiwa 60 wa kuripuwa mabomu kwenye magari baada ya msako kwenye maziko karibu na mahala ambapo kikosi madhubuti cha wanajeshi 5,000 wa Marekani na Iraq kinaendesha msako wa nyumba hadi nyumba kusaka vikosi vinavyojulikana kuwa vya vifo.

Jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani limesema wale waliokamatwa katika msako huo inadhaniwa kuwa wana mafungamano na kundi la siasa kali la Kiislam la Al Qaeda nchini Iraq ambalo limeasisiwa na Osama bin Laden na ambalo limeuwa mamia ya wananchi nchini Iraq.