1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Silaha na chakula vyakutwa vimefichwa na wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6p

Nchini Iraq jeshi la Marekani limesema kuwa jeshi lake na lile la Iraq yanayosaka wapiganaji wa chini kwa chini yamegundua eneo kubwa la maficho chini ya ardhi, silaha na chakula ambacho hakijatayarishwa, vimefukiwa katika jimbo la Al – Anbar.

Kugundulika huko vitu hivyo vilivyofichwa katika eneo ambalo hapo kabla lililkuwa la uchimbaji wa mawe, magharibi ya mji wa Baghdad, ni pamoja na simu kadha za mkononi.

Majeshi ya Iraq wakati huo huo yamesema kuwa yamemkamata mtu anayetuhumiwa kuwa ni gaidi Mullah Mehdi, anayeelezwa kuwa ni msaidizi wa mpiganaji maarufu Abu Musab al- Zarqawi.

Jana Jumamosi kikao cha kwanza cha bunge la jimbo la Wakurdi kilifanyika katika mji wa kaskazini wa Arbil.

Wakurdi wa Iraq wanafanya asilimia 20 ya wakaazi wote wa Iraq wanaokadiriwa kuwa milioni 26.

Waziri wa elimu wa Iraq amesema kuwa mishahara kwa ajili ya waalimu wa vyuo vikuu vya Iraq itaongezwa mara dufu mwezi ujao ili kuzuwia waalimu hao kukimbilia nchi za nje.

Tangu mwaka 2003 waalimu 49 wameuwawa ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye ameuwawa siku 10 zilizopita.