1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Kundi linalohusishwa na al Qaeda ladai kuhusika la mashambulizi kadha ya kujilipua nchini Iraq leo.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFN9

Kundi linalohusishwa na Al Qaeda nchini Iraq linaloongozwa na mpiganaji mzaliwa wa Jordan Abu Musab al-Zarqawi limedai kuhusika na mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyotokea leo mjini Baghdad.

Kiasi cha watu 15 wameuwawa na wengine 35 wamejeruhiwa katika mashambulio mawili ambayo yalilengwa kwa magari ya doria ya polisi katika barabara kuu mjini humo.Afisa wa wizara ya mambo ya ndani amesema kuwa idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka. Mabomu hayo yalifyatuliwa katika mtaa ulio na shughuli nyingi. Mashambulio hayo ya hivi karibuni yamekuja siku moja baada ya milipuko kadha kutokea sehemu mbali mbali nchini Iraq.