1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Kundi linalohusiana na al-Qaeda ladai kuhusika na shambulizi.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2F

Kundi linalohusiana na al Qaeda limedai kuhusika na shambulio la kujitoa muhanga katika lori nchini Iraq jana Jumapili ambalo limeuwa watu kiasi ya 50.

Katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Internet, kundi hilo linalojiita la taifa la Kiislamu nchini Iraq limesema kuwa shambulio hilo lililofanyika katika mji wa kaskazini wa Makhmour limelenga makao makuu ya jeshi la taifa la majeshi ya Wakurd ya Peshmerga.

Makhmour uko nje kidogo ya jimbo la Wakurd nchini Iraq. Bomu jingine lililolipuka katika gari jana Jumapili mjini Baghdad , limeuwa kiasi watu 11 na kuwajeruhi wengine 43.