1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. EU yaahidi fedha zaidi kwa ujenzi mpya wa Iraq.

10 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5C

Ujumbe wa umoja wa Ulaya umekwenda mjini Baghdad kujitayarisha kwa ajili ya mkutano juu ya ujenzi mpya wa Iraq baadaye mwezi huu. Kamishna wa masuala ya kigeni wa umoja wa Ulaya Benita Ferrero-Waldner ametoa ahadi ya kutoa Euro milioni 200 nyingine, na kusema kuwa umoja huo unapanga kufungua ofisi mjini Baghdad.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Luxembourg na Uingereza, Jean Asselborn na Jack Straw, wamesema kuwa Ulaya sasa imeungana kuisaidia Iraq, miaka miwili baada ya mataifa ya umoja wa Ulaya kugawika juu ya vita vya uvamizi dhidi ya Iraq vilivyoongozwa na Marekani.