1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock ataka Israel isitishe ujenzi wa makazi ya walowezi

Sylvia Mwehozi
7 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock hapo jana aliitolea wito Israel kusitisha miradi ya makaazi ya walowezi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi, wakati wa mazungumzo mjini Tel Aviv.

https://p.dw.com/p/4kNk6
Baerbock na Katz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na waziri wa mambo ya nje wa Israel -Israel KatzPicha: GIL COHEN-MAGEN/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock hapo janaaliitolea wito Israel kusitisha miradi ya makaazi ya walowezikwenye eneo la Ukingo wa Magharibi, wakati wa mazungumzo mjini Tel Aviv.

Kabla ya mazungumzo hayo, Baerbock alizuru Saudi Arabia na Jordan, katika ziara yake ya Mashariki ya Kati ya kuhamasisha usitishwaji mapigano, kurejeshwa mateka na misaada zaidi kwa Gaza.

Navyo vikosi vya Israel vimeonekana kuondoka katika mji wa Jenin na makambi mawili ya wakimbizi katika eneo inalolikalia kimabavu la Ukingo wa Magharibi baada ya operesheni kubwa ya kijeshi ya karibu siku 10 iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa.

Katika hatua nyingine mwanamke wa Marekani mwenye asili ya Uturuki ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Ijumaa alipokuwa akiandamana kupinga upanuzi wa makazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi.