1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Baerbock akatiza ziara baada ya droni ya Urusi kuonekana

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelazimika kukatisha ziara yake mjini Mykolaiv nchini Ukraine, baada ya ndege ya droni ya kijasusi ya Urusi kuonekana.

https://p.dw.com/p/4crpq
Baerbock mjini Mykolaiv
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelazimika kukatisha ziara yake mjini Mykolaiv nchini Ukraine, baada ya ndege ya droni ya kijasusi ya Urusi kuonekana. Baerbock alikuwa ziarani katika mji huo wa Mykolaiv mwishoni mwa juma hili, wakati yeye na baadhi ya maafisa katika ujumbe wake walipoamuriwa kurejea kwa haraka katika gari la kiusalama, kufuatia kuonekana kwa ndege ya droni ya Urusi.

Soma: Ukraine yaihimiza Ujerumani kuipatia makombora ya Taurus

Kabla ya mkasa huo, Baerbock alieleza kuwa Ujerumani itatoa nyongeza ya euro milioni 100 kama msaada wa kibinadamu kwa Ukraine kusaidia usambazaji wa maji, hospitali na makaazi.

Waziri Baerbock alisema kuwa licha ya Putin kuendeleza kitisho kwa raia wa Ukraine, lakini hakuna shambulio litakalo haribu mapambano yao ya kuishi.

Mji wa Mykolaiv, uko karibu kilometa 130 kuelekea mashariki mwa Odessa na kilomita 65 kutoka Bahari Nyeusi. Ujerumani inatarajiwa kuandaa mkutano wa kimataifa wa ujenzi mpya wa Ukraine mnamo mwezi Juni mjini Berlin.