1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock akaribisha 'suluhisho' la kesi ya Assange

25 Juni 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amekaribisha mpango wa makubaliano ya kukiri makosa wa mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange pamoja na Marekani.

https://p.dw.com/p/4hUhM
Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock Picha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Akijibu swali la mwandishi wa habari mjini Jerusalem Baerbock amesema amefurahishwa na suhuhu ya kesi hiyo ambayo imejadiliwa kwa hisia sana ulimwenguni pote na kuwagusa watu wengi.

Makubaliano hayo kimsingi yatamruhusu Assange ambaye alikuwa gerezani Uingereza kuhusiana na mzozo wa miaka mingi, kuachiliwa kwa kukiri kosa katika mahakama ya Marekani.

Assange aachiliwa kutoka gereza la Berlmash huko Uingereza.

Marekani inamshutumu Assange kwa kuiba na kuchapisha nyaraka za siri kwenye operesheni za kijeshi za Iraq na Afghanistan na hivyo kudaiwa kuviweka hatarini vyombo vya usalama vya Marekani.