1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bachelet aataka haki za wanawake ziheshimiwe Afghanistan

1 Julai 2022

Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameutaka utawala wa Taliban kuheshimu haki za wanawake na wasichana nchini Afghanistan

https://p.dw.com/p/4DXMO
Russland-Ukraine Krieg | UN-Hochkommissarin für Menschenrechte  Michelle Bachelet
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Michelle Bachelet amedai kwamba haki za wanawake hao na wasichana zinakiukwa pakubwa katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana kwa miongo kadhaa.

Akizungumza mbele ya mdahalo wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Bachelet amesema wanawake wanakabiliwa na njaa, udhalilishaji, ukosefu wa ajira, kutoruhusiwa kwenda sehemu fulani, wanawekewa marufuku ya baadhi ya mavazi na elimu ya sekondari ya wasichana milioni 1.2 imesitishwa. 

Taliban ilichukua mamlaka kwa mara ya pili nchini Afghanistan mwezi Agosti mwaka uliopita baada ya vikosi vya kimataifa vilivyokuwa vinaiunga mkono serikali kuondoka nchini humo.