1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuiomba China mkopo wa dola bilioni moja

6 Oktoba 2023

Rais wa Kenya William Ruto ataiomba China mkopo wa dola bilioni moja ili kukamilisha miradi iliyokwama ya ujenzi wa barabara.

https://p.dw.com/p/4XCwK
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia viongozi mbalimbali walioshiriki mkutano wa masuala ya hali ya hewa barani Afrika uliofanyika Kenya. Kiongozi huyo anataka kuiomba China kuwakopesha ili kumalizia baadhi ya miradi nchini mwake.
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia viongozi mbalimbali walioshiriki mkutano wa masuala ya hali ya hewa barani Afrika uliofanyika Kenya. Kiongozi huyo anataka kuiomba China kuwakopesha ili kumalizia baadhi ya miradi nchini mwake.Picha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Naibu wa rais Rutto, Rigathi Gachagua amesema hayo leo na kuongeza kuwa Ruto atatoa ombi hilo wakati wa ziara yake nchini China baadaye mwezi huu.

Gachagua amesema wakipata dola bilioni moja, basi wawalipa wanakandarasi madeni yao ili waweze kuendelea na ujenzi wa miradi.

Mikopo ya China kwa Kenya ambayo hadi sasa ni zaidi ya dola bilioni nane, ilitumika ya utawala wa rais wa zamani Uhuru Kenyatta kujenga miundo mbinu kama barabara. Lakini miradi mingi ilikwama baada ya waliopewa kandarasi kuondoka kwa sababu ya malimbikizi ambayo hayajalipwa.

Mpango huo wa Rais Ruto unakwenda kinyume na msimamo wake kuhusu madeni ya China hasa wakati walipokuwa wakifanya kampeni kuingia madarakani ambapo muungano wake unaotawala sasa ulikosoa ukopeshaji uliokuwa ukifanywa na utawala wa mtangulizi wake