1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Azerbaijan yatoa waranti wa kukamatwa kiongozi wa Karabakh

1 Oktoba 2023

Azerbaijan leo imetoa waranti wa kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa vuguvugu la kujitenga kwa jimbo la Nagorno-Karabakh, Arayik Harutyunyan.

https://p.dw.com/p/4X1Ko
 Konflikte in Berg-Karabach
Azerbaijan inamtuhumu Arayik Harutyunyan kwa kuamuru mshambulizi dhidi ya mji wake wa Ganja wakati wa vita vya mwaka 2020 Picha: Valery Sharifulin/ITAR-TASS/imago images

Hiyo ni sehemu ya kampeni yake ya kuwachukulia hatua wale walioongoza mapambano dhidi ya serikali mjini Baku.

Hayo yameelezwa leo mchana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Azerbaijan siku kadhaa tangu maafisa wa nchi hiyo walipomkamata kiongozi mwengine wa vuguvugu la Waarmenia wa jimbo la Karabakh, Ruben Vardanyan.

Vardanyan aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Nagorno Karabakh  hadi mwanzoni mwa mwaka huu alitiwa nguvuni siku ya Jumatano akijaribu kukimbia kuelekea Armenia pamoja na makundi mengine ya watu waliolihama jimbo la Karabakh.

Waranti wa kutafutwa kwa Harutyunyan unahusiana na madai kwamba alihusika na mashambulizi ya makombora yaliyoulenga mji wa Azerbaijan wa Ganja, wakati wa vita vya mwaka 2020 vya kuwania jimbo la Nagorno Karabakh kati ya Armenia na Azerbaijan.