1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan yataka Armenia kuondosha wanajeshi N. Karabkh

19 Septemba 2023

Azerbaijan inataka kuondolewa kwa vikosi vya Armenia katika eneo la Nagorno-Karabakh, baada ya Armenia kutangaza kuanzisha oparesheni ya kupambana na ugaidi inayoyalenga maeneo ya kijeshi ya Armenia.

https://p.dw.com/p/4WYvy
Symbolbild Konflikt Bergkarabach
Picha: Artem Mikryukov/REUTERS

Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema oparesheni hiyo ilianza saa chache baada ya wanajeshi wanne na raia wawili kufa katika mripuko wa mabomu ya kutegwa ardhini huko Nagorno-Karabakh.

Hata hivyo, Azerbaijan imesema imefungua njia za kiutu kwa wasio wapiganaji katika eneo hilo ili kukimbia mapigano yaliyoanza.

Soma zaidi: Nagorno-Karabakh yamchagua rais mpya

Urusi imezitaka Azerbaijan na Armenia kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita ya Karabakh na kukomesha umwagaji damu na kufuata demokrasia.

Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa kujaribu kuanzisha kampeni ya mauaji ya kikabila huko Karabakh.

Umoja wa Ulaya umelaani kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, na umeitaka Azerbaijan kusitisha mara moja operesheni yake.