1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan yafanya mazungumzo ya amani na waasi wa Armenia

21 Septemba 2023

Azerbaijan imefanya mazungumzo ya amani na waasi wa Armenia wanaotaka kujitenga. Mkutano huo unajiri wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya pia kikao cha dharura kuhusu mapigano hayo yaliyozuka wiki hii.

https://p.dw.com/p/4Wd9A
Aserbaidschan Baku | Präsident Ilham Alijew hält Fernsehansprache
Picha: Press Service of the President of Azerbaijan Ilham Alijew/REUTERS

Kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa, Azerbaijan imetangaza kuchukuwa udhibiti wa jimbo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, baada ya wapiganaji wenye asili ya Armenia kuweka chini silaha kufuatia kitisho cha kukabiliwa na operesheni kali ya kijeshi. 

Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan alitangaza taarifa hiyo ya ushindi katika hotuba kwa taifa iliyorushwa kupitia televisheni. 

Azerbaijan yasitisha operesheni baada ya Waarmenia kujisalimisha

Jana waasi wa Armenia na Azerbaijan walifikia makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo tayari yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 200 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 400. Hii leo, milio kadhaa ya risasi imesikika katika ngome ya watu wanaotaka kujitenga huko Nagorno-Karabakh.