1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Azerbaijan yadai kumkamata kamanda wa wapiganaji wa Nagorno

29 Septemba 2023

Mamlaka za usalama nchini Azerbaijan zimeeleza leo kuwa zinamshikilia Davit Manukyan, kamanda mkuu anayeshukiwa kujihusisha na shughuli za "kigaidi" katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4Wyoa
Armenien Geflüchtete Berg-Karabach Aserbaidschan
Maelfu ya Waarmenia waliokuwa wakiishi Nagorno Karabakh wameondoka baada ya Azerbaijan kuchukua udhibiti kamili wa jimbo hilo. Picha: DAVID GHAHRAMANYAN/REUTERS

Manukyan, ni naibu kamanda mkuu wa kikosi cha jamii ya Waarmenia wanaotaka kujitenga.

Zaidi ya robo tatu ya wakazi 120,000 wa Nagorno-Karabakh wameondoka na kuelekea Armenia baada ya Azerbaijan kuchukua udhibiti kamili wa eneo hilo. Serikali ya Armenia imesema idadi ya wakimbizi hao imefikia sasa watu 93,000.

Kuna hatari ya mzozo huo uliodumu kwa miongo mitatu kuwa na mwelekeo wa kidini hasa ikizingatiwa kuwa Waarmenia ni Wakristo wa madhehebu ya Orthodox, wakati idadi kubwa ya raia wa Azerbaijan ni Waislamu.