1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan inataka mazungumzo na Armenia bila Magharibi.

21 Novemba 2023

Serikali ya Azerbaijan imesema inapendelea kuwa na mazungumzo ya amani na jirani yake Armenia bila kuwepo upatanishi wa mataifa ya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4ZGZP
Aserbaidschan | Präsident Ilham Aliyev
Picha: Azerbaijani Presidency/AA/picture alliance

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa leo hii na mshauri wa rais wa Azerbaijan Hikmet Hajiyev.Hayo yanajiri wakati leo hii, Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev ameishutumu Ufaransa kwa kuchochea vita vipya katika ukanda wa Caucasia kutokana na vitendo vya Paris kuwapa silaha Armenia.Katika kipindi cha miongo mitatu, Azerbaijan na Armenia zimepigana vita viwili katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, linalotambulika kimataifa kama sehemu ya Azerbaijan lakini ambako wanaishi idadi kubwa ya jamii ya watu wa kabila la Armenia.Baku ilichukua tena udhibiti wa eneo hilo mwezi Septemba baada ya opereshani kubwa ya kijeshi, iliyopelekea takriban watu 120,000 ya eneo hilo kuondoka na kuelekea Armenia.