1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AUGSBURG. Hukumu ya kifungo kwa naibu waziri wa zamani

12 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElX

Mahakama ya Augsburg kusini mwa Ujerumani imemuhukumu naibu wa waziri wa zamani katika wizara ya ulinzi bwana Holger Pfahls kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu gerezani.

Bwana Pfahls alikabiliwa na kesi ya rushwa ma kukwepa kulipa ushuru.

Bwana Holger Pfahls alikiri mbele ya mahakam hiyo kwamba alipokea kiasi cha Euro milioni mbili katika mpango wa vifaru 36 kwa Saudi Arabia mwaka wa 1991 na kisha kushindwa kutoa habari kwa idara ya kodi ya mapato juu ya fedha hizo.

Wiki mbili zilizopita kansela wa zamani Helmut Kohl aliiambia mahakama katikam ushahidi wake kuwa Holger Pfahls hakuhusika na ushawishi wa aina yoyote katika mpango huo wa vifaru kwa Saudi Arabia.

Pfahls alitiwa nguvuni mjini Paris Ufaransa baada ya kuwakwepa polisi wa Ujerumani kwa miaka mitano.