1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATMIS yakamilisha awamu mpya ya kuondoka Somalia

3 Februari 2024

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kimesema kuwa, awamu ya pili ya kuondoka nchini humo inayowahusisha wanajeshi 3,000 imekamilika baada ya kuchelewa kwa miezi minne.

https://p.dw.com/p/4c0Jv
Uganda Kampala | Meeting zu Somalia
Picha: Ministry foreign affairs Uganda

Serikali ya Mogadishu ilikuwa imeomba usitishaji wa miezi mitatu katika mpango huo uliopangwa kutekelezwa kufikia Septemba mwaka uliopita.Taarifa ya ujumbe wa mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema imekamilisha awamu mbili zenye kujumuisha  askari 3,000. ATMIS ilikabidhi kambi saba za kijeshi kwa serikali inayoungwa mkono kimataifa na kufunga zingine mbili.Awamu mbili za kwanza za kupunguza kikosi hicho, zilishuhudia kupunguzwa kwa wanajeshi 5,000. Kundi la Al-Shabaab lilifurushwa katika miji muhimu ya Somalia kati ya mwaka 2011 na 2012, lakini limesalia kudhibiti maeneo mengi ya vijijini.