1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS:Simitis kuwania Urais wa Umoja wa Ulaya

5 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlt
Waziri Mkuu wa Ugiriki Costas Simitis anaweza kuwa mgombea wa kuchukuwa nafasi ya Romano Prodi wakati kipindi chake cha miaka mitano kama Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya kitakapomalizika hapo mwezi wa Oktoba.

Waziri wa ulinzi wa Ugiriki Iannos Papantonio ameliambia gazeti la kisoshalisti la Ta Nea leo hii kwamba Simitis anaheshimiwa sana ndani ya Umoja wa Ulaya na ana mengi ya kuipatia Ulaya.

Ireland ambayo imechukuwa wadhifa wa Urais wa miezi sita wa Umoja wa Ulaya hapo Januari Mosi inategemewa kupokea maoni kutoka kwa wananchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wakati wa mkutano wa viongozi wa umoja huo wa mwezi wa Juni juu ya nani anayefaa kuchukuwa nafasi ya Prodi.