1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athens:Moto wasababisha kifo cha Mjerumani huko Ugiriki.

22 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJ5

Mtalii wa kijerumani amefariki wakati mamia ya watalii na wakaazi wakilazimika kukimbilia katika fukwe huko kaskazini mwa Ugiriki kufuatia msitu kuwaka moto ulioshindwa kuzuiliwa.

Mjerumani huyo mwenye miaka 41 alizama katika ghuba ya bahari ya Cassandra wakati akijaribu kuogelea kuukimbia moto huo ambao unasemekana umechomwa kutoka katika rasi ya Halkidiki kusini mwa Thessaloniki.

Kiasi cha wazima moto 120 na magari ya kuzimia moto 50 yamekuwa katika harakati za kuuzima moto huo.

Ugiriki imekuwa ikikabiliwa na wimbi la joto linalokuwa linapelekea kuwaka moto kwa msitu katika baadhi ya sehemu nchini humo.