1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athens. Bunge la Ugiriki laidhinisha katiba ya Ulaya.

20 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLE

Bunge la Ugiriki limeidhinisha katiba ya jumuiya ya Ulaya kwa kura 268 dhidi ya 17. Hii inaifanya Ugiriki kuwa mwanachama wa sita wa jumuiya ya Ulaya kuidhinisha katiba hiyo. Katiba hiyo inalenga katika kupunguza hatua za kutoa maamuzi katika jumuiya hiyo iliyopanuliwa na kuwa na wanachama 25 sasa.

Katiba hiyo inahitaji kuidhinishwa na mataifa yote wanachama.