1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu laua watu 15 mashariki mwa DRC

8 Oktoba 2023

Kiasi ya watu 15 wamekufa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya watoto kupeleka nyumbani kwao kifaa cha kuripuka walichokiokota michezoni mwao.

https://p.dw.com/p/4XG3T
DR Kongo Bunagana Truppen der EAC
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Mkasa huo ulitokea Ijumaa jioni katika kijiji cha Kyangitsi kilichopo eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Afisa mmoja kutoka katika asasi za kiraia katika eneo hilo, Telesphore Mitondeke, amesema wakaazi wa huko ndio walioweza kubaini kuwa bomu limeripuka baada ya mkasa.Kwa makadirio ya majuma mawili yaliyopita, eneo hilo limekuwa la mapigano kati ya vikundi vya wenyeji wenye silaha vinavyogombea udhibiti wa vijiji, ambapo tayari maeneo mengi yameingia mikononi mwa kundi lijiitalo Wazalendo.