1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lauwa Wapalestina wawili Ukingo wa Magharibi

19 Juni 2023

Jeshi la Israel limewaua Wapalestina wawili na kuwajeruhi wengine wasiopungua 28 wakati wa makabiliano makali yaliyozuka baada ya jeshi la Tel-Aviv kuanzisha msako mjini Jenin katika Ukingo wa Magharibi

https://p.dw.com/p/4SkTL
Westjordanland | Israelischer Militäreinsatz in Jenin
Picha: Nedal Eshtayah/AA/picture alliance

Jeshi la Israel limewaua Wapalestina wawili na kuwajeruhi wengine wasiopungua 28 wakati wa makabiliano makali yaliyozuka hii leo wakati jeshi la Tel-Aviv lilipoanzisha msako mjini Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Wapalestina waliouawa hawakutambuliwa mara moja lakini Wizara ya afya ya Palestina imesema mmoja wao alikuwa kijana mdogo. Vyombo vya habari vimeripoti pia kuwa wanajeshi kadhaa wa Israel wamejeruhiwa.

Kundi la wapiganaji la Islamic Jihad limebaini kushiriki katika makabiliano hayo huko Jenin, miongoni mwa maeneo ya kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi ambayo yameshuhudia katika kipindi cha miezi 15 iliyopita, kuongezeka kwa harakati za jeshi la Israel ambayo pia inashuhudia mfululizo wa mashambulizi ya mitaani ya Wapalestina katika miji yake.

Reuters