1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA : Shemegi wa Habyarimana afikishwa mahkamani kwa mashtaka ya mauaji ya halaiki

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVF

Mwanasiasa wa zamani wa Rwanda ambaye pia ni mfanyabishara amefikishwa mahkamani leo hii kwa mashtaka ya kutokomeza kizazi na mauaji kuhusiana na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ya watu zaidi ya nusu milioni nchini mwake.

Kwa mujibu wa waendesdha mashtaka Protais Zigiranyirazo shemegi wa hayati Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda na mwanachama wa kundi lake la siri linalojulikana kama Akazu aliwaamuru wanamgambo wa misimamo mikali kuwauwa watu 48 katika matukio mawili tafauti wakati wa mauaji ya halaiki ya Watutsi walio wachache na Wahutu wa msimamo wa wastani.

Kwa mara ya kwanza kabisa kesi hiyo inamfikisha mahkamani ndugu wa karibu wa familia ya Juvenal Habyarimana.