1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arusha. Ahukumiwa kifungo na mahakama ya UN.

15 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWq

Mahakama ya kimataifa inayoihusu Rwanda imemhukumu kiongozi wa mmoja kifungo cha miaka sita jela baada ya kukiri kosa lake. Mahakama hiyo ya kimataifa imemhukumu Vincent Rutaganira kwa kusaidia kuwauwa Watutsi ambao waliomba hifadhi katika kanisa moja katika jimbo la Kibuye. Mahakama hiyo ya umoja wa mataifa iliundwa ili kuwahukumu watuhumiwa waliopanga njama za mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994.