1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia, Azerbaijan zaelekea kupata suluhu Nagorno-Karabakh

5 Mei 2023

Marekani imesema kwamba Azerbaijan na Armenia zinakaribia kufikia makubaliano ya amani kuhusu mzozo wao katika eneo la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4QwaP
Berg-Karabach Stepanakert | Flagge
Picha: DAVIT GHAHRAMANYAN/AFP

Kwa miongo kadhaa, nchi hizo mbili zimekuwa zikigombania udhibiti wa eneo hilo la milimani linalokaliwa na Waarmenia wengi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema pande hizo mbili zimepiga hatua kubwa katika kushughulikia masuala magumu, wakati wa mazungumzo ya amani wiki hii pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan Jeyhun Bayramov na Waziri wa Mambo ya Nje wa Armenia, Ararat Mirzoyan yaliyofanyika huko Arlington, Virginia.

Soma zaidi: Armenia na Azerbaijan kufanya mazungumzo ya amani

Blinken amesema nchi zote mbili zimekubaliana kimsingi masharti kadhaa na kuonesha dhamira ya dhati ya kuurejesha uhusiano wao katika hali ya kawaida na kumaliza mzozo wao wa muda mrefu.