1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan ataka wapelekwe wanajeshi wa amani Burundi.

20 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFeS

NEW YORK:
Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan ameliita Baraza la
Usalama lipeleke kikosi cha kuhifadhi amani
nchini Burundi. Nchi hiyo ya Afrika ya Kati ina
nafasi nzuri wakati huu kurejeshewa hali yake
ya usalama miaka kmumi baada ya kumalizika vita
vya ndani. Kwa ajili hiyo hadi hapo tarehe 2
April UM utapaswa kupokea dhamana ya hifadhi ya
amani kutoka nchi za UA. Bwana Annan ameshauri
kipelekwe kikosi cha wanajeshi 5,650 cha UM.
Baraza la Usalama la UM litaijadili hali ya
Burundi hapo Jumatatu.