1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan akaribisha kwa Iran kujiunga na marufuku ya silaha za kinyuklea

15 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDJ

NEW YORK: Katika mvutano kuhusu matumizi ya nishati ya kinyuklea kwa shabaha za kuunda silaha, Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan amekaribisha tangazo la serikali ya Teheran kwamba itayari kutia saini ile hati ziada ya kukataza uenezaji wa silaha za kinyuklea. Katika tangazo lake, Bwana Annan ametukuza ahadi hiyo ya Iran kwamba itaendelea kuheshimu masharti ya hati hiyo hata kabla ya kutiwa saini kwake na kusitisha harakati zake zote zilizopelekea kushutumiwa kwake kuwa na niya ya kuunda silaha za kinyuklea. Hati hiyo ziada inawaruhusu wakaguzi silaha wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea kuingia wakati wowote Iran kwwa shabaha ya kukagua miradi yake ya kinyuklea. Marekani imekuwa ikiishutumu Iran kuwa na shabaha ya kuunda silaha za kinyuklea.