1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Uturuki yakubaliana na Israel kubadilishana maji kwa silaha na mitambo ya ulinzi

6 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlf
Serikali ya Israel na wakuu wa uturuki, wamesaini makubaliano ya kubadilishana maji kwa ununuzi wa silaha na mitambo ya ulinzi.
Gazeti la Uingereza Guardian lililotangaza habari hizo, linasema kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali ya Israel itajenga mabomba yenye uwezo wa kusafirisha zaidi ya lita za maji miliyoni hamsini kila mwaka, kwa muda wa miaka ishirni, kutoka mto wa Manavgat wa eneo la uturuki Anatolie.
Uturuki nayo itapata kibali cha kununua vifaru vya jeshi lake na mitambo ya ulinzi inayotumia teknolojia za kisasa, kutoka Israel.
Uturuki ni miongoni miongoni mwa nchi za mashariki ya kati, yenye kuwa na ushirikiano wa kijeshi na Israel.