1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAngola

Angola imesema itatuma wanajeshi DRC

11 Machi 2023

Angola imesema Jumamosi kuwa itatuma wanajeshi katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo baada ya kuvunjika kwa mkataba wa kusitisha mapigano iliyousimamia kati ya vikosi vya serikali na waasi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4OYCg
Portugal | UN Ocean Conference 2022
Picha: João Carlos/DW

Taarifa kutoka ofisi ya rais nchini humo, imesema kuwa lengo kuu la kikosi hicho ni kuhakikisha usalama katika maeneo yanayothibitiwa na waasi na kuwalinda wajumbe walioopewa jukumu la kufuatilia utekelezwaji wa usitishaji wa mapigano.

Angola imesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya mashauriano na Congo na kuongeza kuwa viongozi wengine wa kikanda pamoja na Umoja wa Mataifa wamearifiwa. Hata hivyo, hatua hiyo inahitaji idhini ya bunge ambapo chama tawala ambacho kimekuwa mamlakani tangu miaka ya sabini kina wingi wa kura. Hakuna taarifa zaidi kuhusu ukubwa wa kikosi hicho zilizotolewa.