1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC na DA vyakubaliana kuunda serikali Afrika Kusini

14 Juni 2024

African National Congress, ANC, na Democratic Alliance DA, ambavyo ndiyo vyama vikubwa zaidi katika bunge jipya lililochaguliwa nchini Afrika Kusini, vimefikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

https://p.dw.com/p/4h2RN
Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,Picha: Zhang Yudong/Xinhua/picture alliance

Serikali hiyo ya muungano pia itavihusisha vyama vya Inkatha Freedom Party na Patriotic Alliance.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Afrika Kusini, SABC. Shirika hilo la utangazaji limesema kwa mujibu wa makubaliano hayo, chama cha DA kitachukua nafasi ya Naibu Spika wa Bunge. 

ANC: Makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yamepatikana

Bunge la Afrika Kusini linakutana hii leo kumchagua Rais pamoja na spika na naibu wake, kufuatia uchaguzi mkuu wa Mei 29, ambamo kwa mara ya kwanza chama tawala cha ANC kilishindwa kupata wingi wa kujitosheleza kuunda serikali kivyake.