1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM:Moto wauwa watu 15 katika uwanja wa ndege wa Schiphol,Uholanzi.

27 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEO8

Vyombo vya habari vya Uholanzi vimeeleza kuwa moto uliozuka ndani ya chumba cha mahabusu katika uwanja wa ndege wa Schiphol umesababisha watu 11 kufa.

Mahabusi hiyo katika uwanja huo wa ndege wa Schiphol,mara kwa mara yanatumika kuwahifadhi wahamiaji wanaotakiwa kurejeshwa makwao na wale wanaotuhumiwa kuingiza dawa za kulevya.

Shirika la habari la Uholanzi ANP,limemnukuu msemaji wa wizara ya sheria ya nchi hiyo,akisema watu wengine 15 walijeruhiwa katika mkasa huo.

Bado haijafahamika chanzo cha moto huo.

Msemaji wa uwanja huo wa ndege amesema moto huo ulioanza muda mfupi baada ya usiku wa manane,ulichukua saa tatu kuzimwa.

Hata hivyo safari za ndege hazikuathiriwa na mkasa huo.