1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM : Watuhumiwa 12 kuachiliwa huru

25 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDII

Serikali ya Uholanzi itawaachilia huru abiria wote 12 raia wa India waliokamatwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Marekani iliokuwa ikielekea India hapo jana baada ya kubaini kwamba walikuwa hawapangi shambulio dhidi ya ndege hiyo.

Msemaji wa mwendesha mashtaka Ed Hartjes amesema kutokana na taarifa za watuhumiwa na mashahidi hakuna ushahidi unaoweza kuwasilishwa kwamba watu hao walikuwa katika hatua ya kutaka kutumia nguvu na kwamba uamuzi umefikiwa wa kuwaachilia huru.

Hartjes ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba wafanyakazi wa ndege waliwatilia mashaka watu hao baada ya kuwa wanakabidhiana simu za mkono na kompyuta mpakato wakati wa safari hiyo na kukataa kufuata maelekezo yao.

Usalama umeiamarishwa kwenye viwanja vya ndege duniani kote katika kipindi cha wiki mbili zilizopita baada ya polisi ya Uingereza kusema kwamba wamefichuwa njama ya kuripuwa ndege zinazokwenda Marekani kutokea Uingereza.