1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM Waholanzi waipinga katiba mpya ya Umoja wa Ulaya

2 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7h

Waholanzi wameipinga katiba mpya ya umoja wa Ulaya. Matokeo ya mwanzo yameonyesha kwamba asilimia 60 ya wapigaji kura waliipinga katiba hiyo. Waziri mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende, amesema licha ya Uholanzi na Ufaransa kuikataa katiba ya jumuiya ya Ulaya, kuidhinishwa kwake lazima kuendelee katika mataifa mengine wanachama.

Mataifa tisa tayari yameikubali katiba hiyo, ikiwemo Ujerumani, lakini ni lazima iidhinishwe na mataifa yote 25 wanachama, kabla kuanza kufanya kazi.