1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Ndege haikukabiliwa na shambulio la kigaidi

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIQ

Waziri wa sheria nchini Uholanzi, Piet Hein Donner, amesema kisa cha ndege ya Marekani iliyorudishwa katika uwanja wa ndege wa mjini Amsterdam, muda mfupi baada ya kuondoka, hakihusiki na ugaidi.

Waziri Donner amenukuliwa akisema hakuna dalili za ugaidi dhidi ya ndege ya shirika la Northwest iliyokuwa njiani ikielekea nchini India.

Washukiwa 12 walikamatwa kufuatia kisa hicho.