1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amsterdam. Mtu aliyemuua mtengenezaji wa filamu van Gogh nchini Uholanzi akiri kufanya kitendo hicho.

13 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEv1

Nchini Uholanzi, mkaazi wa nchi hiyo mwenye asili ya Morocco amekiri kumuua mtengenezaji wa filamu Theo van Gogh Novemba mwaka jana. Katika siku ya pili ya kesi yake mjini Amsterdam , Mohammed Bouyeri amekiri kumuua van Gogh wakati akienda kazini. Bouyeri amewaambia majaji kuwa amefanya hivyo kwa mujibu wa kile anachoamini na kwamba anaweza kufanya hivyo tena iwapo atapata nafasi.

Waendesha mashtaka wametaka hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Bouyeri, ambae wanamueleza kuwa ni Muislamu mwenye imani kali ya kidini. Miezi kadha kabla ya kuuwawa , van Gogh alitengeneza filamu kuhusu matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake katika jamii ya Kiislamu.