1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Abiria 12 wa ndege wakamatwa

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIc

Abiria 12 waliokuwa katika ndege ya shirika la Northwest, la Marekani, walikamatwa baada ya rubani wa ndege hiyo kutoa ripoti ya kuwashuku kuwa magaidi kwa tabia yao. Ndege hiyo iliyotokea mjini Amsterdam nchini Uholanzi ikielekea mjini Mumbai, India, ilirudishwa katika uwanja wa ndege wa Schiphol, ilikoondokea.

Abiria hao 12 walitoa simu zao za mkono na mifuko ya plastiki karibu wakati mmoja na kuzifungua simu hizo wakiwa katika ndege, kinyume cha sheria za usafiri.

Ndege hiyo iliyokuwa katika anga ya Ujerumani wakati huo, ilisindikizwa na ndege mbili za kivita za Uholanzi hadi mjini Amsterdam.

Rubani wa ndege hiyo alilazimika kuyamwaga mafuta yote katika bahari ya Kaskazini kama hatua ya usalama kabla kutua.