1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yaituhumu Mali kutochunguza uhalifu wa kivita

13 Aprili 2022

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limewatuhumu viongozi wa Mali kwa kupiga hatua kidogo kuchunguza visa vya uhalifu wa kivita katika jimbo la Sahel.

https://p.dw.com/p/49uGV
Logo der Organisation Amnesty International
Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Shirika hilo limehoji kuwa uvunjifu wa sheria kiholela unaendelea kutokana na visa kama hivyo.

Kwenye ripoti yake, Amnesty International imesema visa vya machafuko na uhalifu wa kivita dhidi ya raia vimeongezeka tangu mwaka 2018 hususan nchini Mali, taifa linalozongwa na machafuko.

Shirika hilo limeainisha visa kadhaa vya mauaji ya watu wengi yanayodaiwa yalifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kidini, vikosi vya Mali na vilevile jeshi la Ufaransa ambalo lilikuwa la kwanza kuingia nchini humo mwaka 2013 kupambana na wanamgambo.