1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Waasi wa M23 waliwabaka wanawake na wasichana

17 Februari 2023

Shirika la Amnesty International limesema waasi wa M23 waliwabaka zaidi ya wanawake 60 na wasichana wakati walipofanya mashambulizi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4Nezm
Kongo I Kanyaruchinya Lager für Binnenvertriebene
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International imesema waasi wa M23 waliwabaka zaidi ya wanawake 60 na wasichana wakati walipofanya mashambulizi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa hiyo iliyochapishwa hii leo imesema walikusanya ushahidi kutoka kwa wahanga 35 na mashuhuda na kuviainisha visa hivyo kama uhalifu wa kivita. Amnesty imesema kwenye ripoti yake ya kurasa tatu kwamba wanawake hao walibakwa kati ya Novemba 21 na 30.

Umoja wa Mataifa uliarifu wiki iliyopita kwamba waasi hao waliwanyonga watu 171 na kuwabaka wanawake 27 na wasichana katika makazi ya mji wa Kishishe, ambao ni mkubwa katika jimbo la Kivu Kaskazini mnamo mwezi Novemba. Tangu mwishoni mwa mwaka 2021, waasi hao walikamata eneo kubwa kwenye jimbo hilo na kuukaribia mji wa Goma, hatua iliyosababisha wengi kuyakimbia makazi yao.