1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN:Mtandao wa Al-Qaeda walaumiwa mashambulio

12 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJ9

Maafisa nchini Jordan wamesema mashambulio matatu ya bomu yaliyofanywa katika hoteli mjini Amman mapema wiki hii ni kazi ya mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda nchini Iraq.Naibu waziri mkuu wa Jordan,Marwan al Muasher alipozungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema,uchunguzi iliyofanywa umeonyesha kuwa kikundi kinachoongozwa na mwanamgambo Musab al-Zarqawi ambae ni mzaliwa wa Jordan,ndio kilichohusika na mashambulio yaliyouwa watu 57,wengi wao wakiwa raia wa Jordan.Muasher hakutaja uraia wa washambuliaji waliojitolea muhanga lakini amesema watu hao walitokea ngámbo.