1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Aliyevujisha nyaraka za siri Marekani afikishwa mahakamani

14 Aprili 2023

Kijana aliyekamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani akishukiwa kwa uvujishaji mkubwa wa nyaraka za siri amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ya jinai yanayomkabili

https://p.dw.com/p/4Q5MA
USA John Joseph Moakley Gericht in Boston
Picha: Marc Vasconcellos/The Enterprise/USA TODAY Network/IMAGO

Jack Teixeira mwenye umri wa miaka 21 na mfanyakazi wa kamandi ya kikosi cha ulinzi wa anga ya Marekani alikamatwa jana Alhamisi baada ya wiki nzima ya uchunguzi juu ya kuvuja kwa nyaraka nyingi za siri ikiwemo kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Soma pia: Pentagon yamnasa mtu anayeshukiwa kuvujisha nyaraka za siri

Wizara ya Sheria ya Marekani inatazamiwa kuainisha kesi ya jinai inayomkabili na kumfungulia mashtaka chini ya sheria ya ujasusi inayoainisha kuwa ni kosa kuvujisha taarifa za ulinzi wa taifa

Waendesha mashtaka wanaamini kijana huyo ambaye pia ni mtaalamu wa teknolojia alikuwa kiongozi wa kundi la mawasiliano kwenye mtandao ambako nyaraka hizo za siri zilisambazwa.