1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bernard Membe amefariki dunia

12 Mei 2023

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernerd Membe amefariki dunia hii leo katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es salaam.

https://p.dw.com/p/4RHj0
Tansania Bernard Membe erhält seine CCM-Mitgliedskarte in Chiponda Rondo in Lindi, von Shaka Hamdu Shaka
Picha: Salma Mkalibala/DW

Taarifa za awali zilieleza  kwamba alipata matatizo ya kupumua na kupelekwa hospitali alfajiri; leo Ijumaa na baadae kufariki. Membe alizaliwa mwaka 1953 na alikuwa mwanasiasa nchini Tanzania aliyewahi kushikilia nafasi mbali mbali ikiwemo waziri wa mambo ya nje kuanzia mwaka 2007  mpaka 2015. Alikuwa pia mbunge wa jimbo la Mtama  kuanzia mwaka 2000 hadi 2015. Vile vile alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 akipeperusha bendera ya chama cha upinzani cha ACT Wazalendo baada ya kukihama chama tawala cha CCM.