1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi DRC atuhumiwa kwa uhaini

Jean Noël Ba-Mweze
21 Agosti 2023

Muungano wa vyama vinavyotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umemtuhumu aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, CENI, iliyomuingiza Rais Félix Tshisekedi, Corneille Nangaa kwa uhaini.

https://p.dw.com/p/4VOyg
Demokratische Republik Kongo | symbolisches Wahllokal in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Haya yamejiri baada ya Corneille Nangaa, ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha upinzani cha ADCP kuikimbia nchi yake na kwenda uhamishoni nchini Ghana, akidai kutishiwa maisha yake na utawala wa Tshisekedi.

Corneille Nangaa, ambaye tayari amejitangaza kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika hapa Disemba 20, alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuuondosha utawala wa Felix Tshisekedi, akikosoa usimamizi mbaya wa masuala ya kitaifa, uzembe na hatua zinazochukuliwa bila mipango katika sekta ya usalama.

Ulazima  wa kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi.

Demokratische Republik Kongo | Wahllokal in Kinshasa
Makalani wa uchaguzi nchini DRCPicha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Lakini kauli yake ambayo inayowashtua zaidi wafuasi wa Rais Félix Tshisekedi ni kudhaniwa kuwepo kwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Rwanda la FDLR katika Kikosi Maalum cha Ulinzi wa Rais.

Muungano wa vyama vinavyotawala, USN, unasema matashi hayo ni usaliti na hivyo Corneille Nangaa lazima afikishwe mbele ya mahakama ya kijeshi kwani anasambaza propaganda ya utawala wa Rwanda. Thierry Monsenepo ni msemaji wa USN anasema "Corneille Nangaa tayari ameuvuka mstari mwekundu kwa kuisaliti nchi yake huku akijiweka sawa na hoja ya Paul Kagame.

Kusema kuwa jeshi letu linashirikiana na FDLR ni uongo mtupu unaoungwa mkono na Kigali Ili kuhalalisha unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Rwanda kwenye ardhi yetu. Kuona ni mmoja wa viongozi wa zamani ndiye anasambaza ujumbe kama na huo sherti kumtakia tu ghadhabu zote za mababu zetu."

Hofu ya usalama wa mtuhumiwa Corneille Nangaa.

Corneille Nangaa amesisitiza kwamba anahofia usalama wake kwani vitisho dhidi yake vilikuwa vingi baada ya kuyaonya mamlaka kuhusu hali mbaya ya nchi uhususan ile ya kiusalama. Na hivyo hayuko tayari kurejea hapa nchini hadi hali ya kisiasa itakapoimarika.

Upande mwengine Nangaa aligusia hali ambamo wapinzani kadhaa hukamatwa na kutiwa mbaroni pia wengine kuwawa kama vile mubunge Chérubin Okende, msemaji wa Ensemble pour la République, chama cha Moïse Katumbi aliyetekwa nyara na kuwawa hivi karibuni.

Soma zaidi:Guterres asema MONUSCO inakaribia kuondoka Kongo

Tukumbushe kwamba Corneille Nangaa ndiye aliongoza tume ya uchaguzi wakati wa uchaguzi wa rais wa Disemba 2018 na hivyo katangaza Januari 2019 matokeo na kumfaya Félix Tshisekedi kuwa raïs wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lakini hadi sasa mpinzani Martin Fayulu hajawahi kukukubali ushindi huo wa Tshisekedi na hivyo anaendelea kujitaja kuwa rais mteule wa Kongo.

DW Kinshasa