1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Aliyekuwa kiongozi Pakistan Pervez Musharraf kuzikwa leo

7 Februari 2023

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa Pakistan Pervez Musharraf anatarajiwa kuzikwa hii leo. Musharraf ambaye alikimbilia Dubai mwaka 2016, alifariki Jumapili wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 79.

https://p.dw.com/p/4NBIJ
Pakistan Ex-Präsident Pervez Musharraf
Picha: B.K. Bangash/AP/picture alliance

Hayati Musharraf aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Wakati wa uongozi wake alikuwa mshirika wa Marekani katika vita vya kupambana na ugaidi.

Licha ya kutotolewa tamko rasmi juu ya mazishi yake, maafisa wa kijeshi ambao hawakutaka kutajwa wamesema Musharraf anatarajiwa kuzikwa leo mjini Karachi.

Musharaf alitwaa mamlaka mnamo mwaka 1999  bila ya umwagaji  damu na kwa wakati mmoja alivaa kofia za mkuu wa jeshi na rais wa nchi. Musharraf alisimamisha katiba ya nchi mara mbili na alilaumiwa kwa kuchakachua matokeo ya kura ya maoni.