JamiiUswidi
Aliyechoma Quran nchini Sweden auawa kwa risasi
30 Januari 2025Matangazo
Salwan Momika ambaye alikuwa mkimbizi kutoka Iraqi na mwanaharakati anayeupinga Uislamu ameuawa saa chache kabla ya kufika mahakamani kusikiliza hukumu juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na matendo yake ya kuichoma moto Quran.
Mwaka 2023 mwanaume huyo alifanya matukio kadhaa ya kuzichoma moto na kuzinajisi nakala za Quran katika kile alichosema kuwa ni kuilinda jamii ya Sweden dhidi ya mafundisho ya kitabu hicho cha kidini.
Matendo yake yalizusha ghadhabu na ukosoaji kutoka mataifa mengi ya Kiislamu na wakati mwingine mamia ya watu waliandamana kulaani matukio hayo. Polisi imesema watu watano wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.