1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUswisi

Ubalozi wa Sweden mjini Baghdad wachomwa moto

20 Julai 2023

Mamia ya waandamanaji wamevamia na kuwasha moto kwenye ubalozi wa Sweden nchini Iraq usiku wa kuamkia leo kuelekea tukio la uchomaji kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Quran.

https://p.dw.com/p/4U9vK
Themenpaket | Irak Protest Botschaft Schweden
Picha: AHMED SAAD/REUTERS

Tukio hilo la kuchoma kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Quran limepewa kibali na mamlaka za Sweden kufanyika kwenye mji mkuu wa taifa hilo, Stockholm.

Duru zinasema moshi umeonekana ukifuka kutoka majengo ya ubalozi wa Sweden mjini Baghdad na makundi ya waandamanaji bado wako kwenye eneo hilo. Idadi kubwa ya polisi wa kutuliza ghasia wametawanya kurejesha utulivu.

Inaarifiwa waandamanaji hao wameghadhabishwa na uamuzi wa polisi ya Sweden kutoa kibali cha mkusanyo mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm, ambako waandaaji wanapanga kuchoma moto Quran pamoja na bendera ya taifa ya Iraq.

Tukio kama hivyo wiki kadhaa zilizopita lilizusha ghadhabu miongoni mwa waislamu duniani.