1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliou Cisse: Timu ya Afrika itachukua Kombe la Dunia

26 Novemba 2022

Kocha wa Senegal Aliou Cisse amesema anaamini timu ya Afrika itaibuka na ubingwa kombe la dunia safari hii baada ya timu yake kuifunga Qatar mabao matatu kwa moja, katika mchuano wa kundi "A"

https://p.dw.com/p/4K6Ek
Fußball-WM Katar 2022 | Katar vs Senegal
Picha: Petr Josek/AP Photo/picture alliance

Hakuna timu ya Afrika iliwahi kuvuka katikla hatua ya robo fainali katika kombe la dunia na ni Cameroon na Ghana tu ndio zilizowahi kufikia hatua hiyo. Cisse anaamini mfulizo wa matokeo ya kushangaza hadi wakati huu nchini Qatar yanathibitisha kuwa "mambo yamebadilika" katika soka la dunia na haoni sababu kwa nini mwaka huu usiwe wa Afrika.

Kocha huyo ambae alikuwa sehemu ya timu ya Senegal iliyoisumbua Ufaransa kwenye hatua za mchuano wa robo fainali nchini Japan na Korea Kusini miaka 20 iliyopita amenukuliwa na vyombo vya habari akisema ana imani kuwa  taifa la Afrika litaibuka na ushindi na karata yake kaitupa kwa Senegal.

Kocha wa Senegal Aliou Cisse asema hakuna miamba ya soka katika Kombe la Dunia la sasa

Fußball-WM Katar 2022 | Katar vs Senegal
Wachezaji wa Senegal wakishangilia ushindiPicha: AFP

Amesema timu zote ambazo zipo katika mchuano huo kwa uwezo zinastahili kuwepo katika mashindano hayo. Na sio kama miaka 30 na 35 iliyopita kwamba samaki wakubwa wanawala wadogo.

Senegal walipata goli la mwanzo kupitia kwa Boulaye Dia katika dakika ya 41 ya muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Famar Diedhiou akatia wavuni bao la pili na la tatu likafungwa na Bamba Dieng bao lililowahakikishia mabingwa hao wa Afrika pointi tatu muhimu katika kundi lao A na kuyaweka hai matumaini yao ya kufuzu katika raundi ya mtoano ya mashindano hayo.

Qatar ndiyo inakuwa timu ya kwanza kuuaga mchuano wa Kombe la Dunia

Qatar wamefungiwa bao la kufutia machozi  na Mohammed Muntari kwenye dakika ya 78. Senegal ilifungwa 2-0 na Uholanzi katika mechi yao ya ufunguzi. Wakati huo huo, Qatar ndiyo inakuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo licha ya kuwa hawajacheza mechi moja ya mwisho dhidi ya Uholanzi. Timu nyengine ailiyoko katika kundi hilo ni Ecuador, ambayo ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Qatar katika mechi ya kwanza.

Soma zaidi:Kocha wa Ghana alalamikia Penalti ya Ronaldo

Katika michuano mingine katika kundi B, England imetoka suluhu tasa na Marekani, Iran imechapa Wales bao mbili na kundi A Uholanzi imetoka sare ya moja kwa moja na Ecuador. Ratiba ya leo kwa kundi D, Tunisia na Australia, Poland na Saudi Arabia kwa kundi C, Ufaransa na Denmark kundi D na mwisho Argentina na Mexico katika za kundi C.

Chanzo: AP