1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria waduwazwa, Ivory Coast wakabwa koo na Sierra Leone

17 Januari 2022

Katika mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika, AFCON yanayoendelea huko Cameroon ambapo Jumapili mabingwa watetezi Algeria walishangazwa na Guinea ya Ikweta walipofungwa goli moja kwa bila.

https://p.dw.com/p/45eSH
Fußball | Africa Cup of Nations | Elfenbeinküste - Sierra Leone
Picha: CHARLY TRIBALLEAU/AFP

Katika mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika, AFCON yanayoendelea huko Cameroon ambapo Jumapili mabingwa watetezi Algeria walishangazwa na Guinea ya Ikweta walipofungwa goli moja kwa bila. 

Kushindwa huku kuliwapelekea kuwa na pointi moja tu kufikia sasa katika kundi lao wakiwa wanaelekea kucheza mechi yao ya mwisho ya kundi watakapovaana na Ivory Coast ambao wenyewe walilazimishwa sare ya dakika za mwisho, baada ya makosa yaliyofanywa na kipa wao, kuwapelekea Sierra Leone kusawazisha na kusababisha mechi yao kuishia sare ya mabao mawili.

Kundi hilo sasa linaongozwa na Ivory Coast iliyo na pointi 4 kisha Guinea ya Ikweta ina pointi 3 Sierra Leone ni wa tatu wakiwa na pointi mbili kisha mabingwa watetezi Algeria wanauvuta mkia wakiwa na pointi moja tu.

Jumatatu kunachezwa mechi nne kwa wakati mmoja, Burkina Faso watakuwa wanapambana na Ethiopia kisha Cape Verde wavaane na wenyeji Cameroon. Malawi watakuwa wanatafuta pointi tatu muhimu kwa Senegal kisha Zimbabwe wacheze na Guinea.