1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Albanese ataka mashtaka ya Assange yasitishwe

30 Novemba 2022

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema kuwa amewaomba binafsi maafisa wa Marekani kusitisha mashtaka dhidi ya mwanzilishi wa tovuti ya WikiLeaks Julian Assange.

https://p.dw.com/p/4KHQa
Julian Assange Weltweite Proteste gegen Finanzindustrie und Krise
Picha: dapd

Assange ambaye ni raia wa Australia, amekuwa akizuiliwa mjini London tangu mwaka 2019 akisubiri uamuzi juu ya ombi la Marekani kumkabidhi kwa kuvujisha siri za jeshi mnamo mwake 2010, kuhusu vita nchini Iraq na Afghanistan.

Kiongozi huyo wa Australia amesema hana huruma na vitendo vingi vya Assange mwenye umri wa miaka 51, lakini amehoji sababu ya kuendeleza hatua za kisheria dhidi yake.

Assange amekuwa akishikiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh mjini London tangu 2019, baada ya kutumikia kifungo kwa kuvunja masharti ya dhamana katika kesi nyingine na kujichimbia kwa miaka kadhaa katika ubalozi wa Ecuardo.